Mashujaa wa Kenya
- Josephine

- Oct 20, 2018
- 1 min read
Updated: Aug 12, 2020
Mlijitolea kupigania uhuru wetu,
bila kutarajia zawadi,
kwa kuonyesha ujasiri,
na kuvumilia mateso,
Ili tuweze kuishi vyema.
Heko kwenu Mashujaa!
twazidi kuwa furahia,
kwa sababu ya historia yenu,
tuna heshima kama nchi,
mlitujengea jina na kutupa kiburi.
Viwango mliviweka juu,
Kweli nyinyi ni wakuu,
wenye busara kwa wingi,
na uwezo wa uongozi,
Kwa vitendo na mienendo.
Twashukuru kila siku,
na kuwakumbuka hii siku,
kwani ahadi zenu mliweka,
ingawa mlivunjwa miyoyo,
hamkuacha kutupigania.
Mlitufunza vyema,
Kwa kuwa mifano njema,
Nasi tunaendelea na ujenzi,
wa taifa letu la Kenya,
kwa njia mlio tueleza, bila kusita.




Comments